HabariSiasa

Waziri Lavrov wa Urusi kukutana na Rais Museveni

Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lavrov amewasili nchini Uganda katika ziara yake ya tatu katika nchi za Afrika, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Russia ametangaza Jumatatu.

Lavrov alilakiwa mjini Entebbe na mwenzake wa Uganda, Jeje Odongo, amesema Maria Zakharova akichapisha picha ya mawaziri hao wawili kwenye mtandao wa Telegram.

Kwa mujibu wa shiriika la habari la Russia TASS, Lavrov anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda Yoweri Museveni leo Jumanne.

Shirika la habari la AFP limewasiliana na maafisa wa Uganda, lakini hawakutoa maelezo zaidi juu ya ajenda ya ziara hiyo.

Jumapili, serikali ya Uganda iliandika kwenye Twitter kwamba Lavrov atakuwa nchini humo kwa ziara ya siku mbili.

“Rais Yoweri Museveni alifanya ziara nchini Russia mwaka wa 2019 na alitoa wito wa kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili, hasa katika sekta za ulinzi na usalama, ushirikiano wa kiuchumi na kiufundi,” serikali iliandika.

Akianza ziara yake ya Afrika mjini Cairo Jumapili, Lavrov aliwahakikishia viongozi wa Misri kwamba makubaliano ya zabuni zao za kununua nafaka ya Russia yatatekelezwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents