Waziri Mkuu Israel apandishwa kizimbani kwa tuhuma za ufisadi

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, alipandishwa tena kizimbani hivi leo kukabiliana na kesi zake ya ufisadi.
Netanyahu anatuhumiwa kwa rushwa, udanganyifu na uvunjaji wa imani kwenye kesi tatu tafauti dhidi yake.
Wakati kesi yake ilipotajwa, mwendesha mashitaka mkuu, Liat Ben-Ari, alisema kwamba Netanyahu alitumia vibaya madaraka kwa maslahi binafsi na kutowa bahashishi kwa vyombo vya habari ili vimsaidie achaguliwe tena.
Kiongozi huyo, mwenye umri wa miaka 71, ni waziri mkuu wa kwanza aliyeko madarakani kushitakiwa katika taifa hilo la Kiyahudi. Wakati huo huo, Rais Reuven Rivlin wa Israel alianza mazungumzo na viongozi wa vyama vya kisiasa, ikiwa ni wiki mbili baada ya uchaguzi mwengine uliozuwa mkwamo wa uundwaji serikali.
Amekutana hivi leo na wawakilishi wa chama cha Likud cha Netanyahu, ikiwa sehemu ya mikutano kama hiyo ya kumsaidia kuamua kiongozi mwenye nafasi ya kuunda serikali ya mseto.

Related Articles

Back to top button