Burudani

Wema awalaumu waigizaji kukaushia suala la Roma, Ray amjibu

Matatizo huja na matatizo mengi na mara nyingi huwa ni kipimo cha upendo katika watu wanaohusika nayo.

Kupotea kwa Roma na wenzake kumesababisha si tu taharuki, bali pia mvurugano wa hapa na pale. Mrembo na muigizaji wa filamu, Wema Sepetu amewashutumu wasanii wenzake wa filamu kuwa hawaoneshi ushirikiano katika mkasa uliotokea kwa Roma.

Ameandika:

This Is Scary… Ni Janga kubwa sana kwa wasanii, kwa wananchi na Kwa Taifa letu kiujumla… Kinachonishangaza ni kuona baadhi ya wasanii wa Bongo movie wamekazana kupost eti wapo kwa Mkuu wa mkoa wakiongelea WaKorea na Waphilipino…. Mlikumbuka kumuuliza Mheshimiwa alipo Roma na Moni…??? Au ndo mambo ya kila mtu anaangalia lake…. Au labda mpaka atekwe msanii wa Bongo movie pia ndo akili itatukaa sawa…??? Oh God help Us Please… Lakini pia wala sitoshangaa hata kama akitekwa msanii wa bongo movie hakuna atakaehangaika within Us zaidi ya wananchi peke yao na watu wetu wa karibu… Tumejawa sana Unafki…!!! All in All namuonea sana huruma Nancy…. Our prayers are with u mama… Inshallah mumeo atapatikana… Tuzidi kumuomba Mungu…..????????????????????????…. Kabla sijasahau, Tuwage tuna hata fikra za kujua tupo kwenye wakati gani na tupost vitu gani….!!! Yaani mtu kapotea siku ya pili mko busy na kupost Wakorea na Waphilipino…?? ???????????? SMH..

Ray Kigosi amelazimika kuwasaidia wenzake kumjibu Wema:

NAFIKIRI NI VEMA MTU KUELEZA HISIA ZAKE JAPO SIO BUSARA KWA MWENYE HISIA HIZO KUZIELEZA BILA WEREDI NAWASIHI WASANII WENZANGU KUPOTEA KWA ROMA ISIWE SABUNI YA KUTAKATISHA UCHAFU WA MTU SOTE TUMESIKITISHWA NA JAMBO HILO NA TUMEONYESHA KWA VITENDO. MIMI NIMEPOST INSHU YA ROMA TANGU JANA USIKU WEMA SEPETU WEWE ULIKUWA HUJAPOST CHOCHOTE TUSEME ULIKUWA HUNA UCHUNGU? ALAFU LEO UNAANDIKA KUWA BONGO MOVIE HAWAPO PAMOJA NA TUKIO LA ROMA HUKU NI KUTUGOMBANISHA NA WANANCHI WANAOTUAMINI. SISI BONGO MOVIE MARA NYINGI SANA TUNAKUWA PAMOJA KWENYE MATUKIO YA BONGE FLEVA TOFAUTI NA WAO. KAMA UNA UGONVI NA MTU HAYO NI MAMBO YAKO BINAFSI ILA USITUFANYE SISI TUONEKANA WABAYA MBELE YA JAMII UTAKUWA KICHAA KAMA USIPOPATA MAUMIVU KWA TUKIO LA ROMA NIMESIKITISHWA SANA POST YAKO @wemasepetu KAMA UNADHANI HUU NI MUDA MUAFAKA WA KUTAFUTIA POINT KATIKA TUKIO LA ROMA MKATOLIKI UMEFELI HILI NI JANGA LETU SOTE. @wemasepetu #(KINA ROMA WAKO WAPI?).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents