Burudani

‘Wema Sepetu na Lulu wanaweza kufanya vizuri Hollywood’ asema staa mkubwa wa filamu

Staa wa filamu ya Going Bongo, Ernest Napoleon amesema Wema Sepetu na Elizabeth ‘Lulu’ Michael wanaweza kufanya vizuri Hollywood.

wema lulu

Akiongea na Bongo5, Napoleon amesema uwezo wa waigizaji hao unaweza kutisha watu kama wakipewa muongozo mzuri.

“Tanzania tuna waigizaji wazuri wengi sana,” amesema. “Watu wengi wakiangalia bongo movie wanaona movie mbovu au vipi. Hilo sio suala la uigizaji, hayo yanakuwa ni mambo mengine ya production yanayofanya filamu iwe mbovu labda filamu imeharakishwa sana.”

Amewataja Lulu na Wema Sepetu kama wasanii wanaoweza kufanya vizuri wakielekezwa mambo ya msingi. Amemfananisha Lulu kama muigizaji wa Marekani, Lindsay Lohan ambao wote walianza kuigiza wakiwa na umri mdogo.

“Kipaji kama cha Wema Sepetu, tayari ana kile kipaji cha kuwa charismatic, cha kupendwa na watu unajua kama kipaji cha Obama kila akiongea tu watu wanamsikiliza, mtu kama Wema ana kipaji kile. Ukiunganisha na uwezo wa kuigiza na akawekwa kwenye project ambayo inamfaa.”

Alimtaja pia Idris Sultan kuwa ana uwezo mkubwa wa kuigiza filamu za kuchekesha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents