Burudani

Wema Sepetu: Nasib Abdul angekuwa mume wangu wa maisha

Jina la Nasib Abdul bado halijatoka kichwani mwa Wema Sepetu!

wpid-wema-akiwa-pembeni-kumsupport-diamond1.jpg

Nasib Abdul ni jina halisi la Diamond Platnumz.

Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 na muigizaji wa filamu alikuwa akijibu swali kwenye kipindi cha Hitzone kupitia kituo cha redio cha Jembe FM cha jijini Mwanza alipoulizwa ni mwanaume gani ambaye alitamani awe mume wake wa ndoa.

“Ni yupi ambaye niliwahi kusema huyu anaweza kuwa wa maisha,” alisema Wema. “Kiukweli alikuwa anaitwa Nasib Abdul,nilishawahi kusema hivyo,” alisisitiza.

Hata hivyo ndoto hiyo iliyeyuka baada ya wawili hao kuachana mwaka jana na Diamond kuhamisha mahaba yake kwa Zari the Bosslady ambaye tayari wana mtoto wa kike, Tiffah.

12145131_446132162256651_1648976670_n

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents