Habari

WHO yaonya kuongezeka kwa usugu wa ugonjwa Gonorrhea

Kama bado huna mtoto na hutaki kuwa mgumba chonde chonce jiepushe na ngono zembe kwakuwa ukijikwaa na ukapata Gonorrhea usishangae ikatengeneza makazi ya kudumu mwilini mwako.

Shirika la afya duniani WHO jana jumatano limesema kuwa ugonjwa huo wa zinaa unaoathiri mamilioni ya watu kila mwaka duniani umeanza kuwa sugu kwa dawa na hivi karibuni unaweza usitibike kabisa.

Shirika hilo limewataka madaktari na serikali kuchunguza gonorrhea isiyotibika kwa antibiotic – ambukizo la bakteria ambalo husababisha maumivu, ugumba, matatizo ya ujauzito na pia vifo wakati wa kujifungua. Pia watoto wanaozaliwa na gonorrhea huwa na asilimia 50 za kuambukizwa machoni na kusababisha upofu.

“Bakteria huyu amekuwa akiendelea kujitengenezea usugu dhidi ya kila dawa tunayotumia,” alisema Dr. Manjula Lusti-Narasimhan, mwanasayansi kwenye kitengo cha shirika hilo cha magonjwa yanayoambukiza kwa njia ya kujamiiana

WHO limesema ugonjwa huo huwapata takriban watu milioni 106 kila mwaka na pia huongeza hatari ya kuambukizwa kwa magonjwa mengine kama virusi vya HIV.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents