Burudani

Wivu wa mapenzi wamponza Blac Chyna, adundwa na Boyfriend wake Kid Buu na kutelekezwa hotelini

Wakiwa katika mapumziko Hawaii , mwanamtindo Blac Chyna akiwa na boyfriend wake rapper Kid Buu wameripotiwa kudundana ngumi.

TMZ wameripoti kutokea kwa tukio hilo huko Hawaii, na imeelezwa majira ya saa tano asubuhi wakiwa katika chumba cha kwenye hotel walioyofikia ya
Ritz-Carlton, Honolulu siku ya jumatatu, waliweza kudundana baada ya Chyna kumlaumu mpenzi wake kumsaliti kimapenzi. yaani Blac Chyna kuzidisha wivu kwa mpenzi wake huyo.

Na vyanzo vingi vimeripoti kuwa Kid Buu alimpiga na kumpigiza mara kadhaa ukutani na baada ya tukio hilo kuonekana kuna mtu aliwapigia Polisi namba 911 na baada ya muda kidogo polisi walifika katika eneo la tukio.

Mbali na kudundwa kote huko Blac Chyna hakupelekwa hospitalini baada ya kuonekana hakuumia sana na baada ya muda kidogo Kid Buu aliondoka hotelini na kupost Clip akiongea kwa lugha ya Kihispani akisema :-
“Don’t f**k with me, I’m a grown man.”  akimaanisha usinizingue tayari nimeshakuwa sasa”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents