Uncategorized

Sahau matokeo ya Sportpesa, Mapinduzi Cup na zile tano za AS Vita, haya ndiyo malengo makuu aliyopewa Patrick Aussems na Simba SC

Patrick Aussems ni raia wa Ubelgiji ambaye kwa muda sasa yupo hapa nchini akifanya kazi yake ya ukocha ndani ya klabu ya Simba akirithi mikoba iliyokuwa imeachwa wazi na Mfaransa, Pierre Lechantre.

Aussems mwenye umri wa miaka 54, alitambulishwa rasmi ndani ya miamba hiyo ya soka ya Tanzania, Julai 19 mwaka 2018 kupitia msemaji wake mkuu, Haji Manara wakati ambao Simba ilikuwa chini ya kocha msaidizi ‘Assistant Coach’ Irambona Masud Juma.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamiko miongoni mwa mashabiki wa Simba kufuatia matokeo mabovu ambayo timu hiyo imeyapata kwenye michuano yake mbalimbali.

Januari 13 mwaka huu 2019, Simba imejikuta ikipata kipigo cha jumla ya mabao 2 – 1 mbele ya matajiri wa jiji la Dar es Salaam Azam FC kwenye mchezo wa fainali ya mapinduzi Cup.

Huku Januari 19, wakipata kichapo kikali na cha fedheha cha magoli 5 – 0 dhidi ya AS Vita Club mchezo wa klabu bingwa Afrika uliyochezwa nchini DR Congo.

Ukiachiambali matokeo hayo hivi majuzi Simba imejikuta ikiyaaga mashindano ya wadhamini wao wa kuu Sportpesa hatua ya nusu fainali dhidi ya Bandari kwa jumla ya mabao 2 – 1 matokeo ambayo hayakutarajiwa na watu wengi.

Wakati wa kutambulishwa kwa Aussems, Haji Manara alisema kuwa Mbelgiji huyo ambaye amepata nafasi hiyo baada ya kupokea ‘CV’ za makocha 57 ni kutokana na ubora wake na wamempa malengo yao kama klabu.

‘’Tumempa malengo, kwanza lengo kuu ni kutetea ubingwa wa ligi kuu wa Vodacom hili lipo wazi, hilo ndilo lengo namba moja,’’ amesema Haji Manara msemaji wa klabu ya Simba wakati akimtambulisha kocha huyo kwa waandishi wa habari.

‘’Lengo namba mbili ni kuiwezesha klabu ya Simba kufuzu hatua za makundi kwenye klabu bingwa Afrika. Kwa hiyo tumeweka lengo tuingie hatua ya makundi Afrika na lutetea ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom.’’

Kutokana na malengo hayo mawili ambayo klabu ya Simba imekubalia na kocha Aussems hata kwenye mkataba wake wake kama alivyosema Manara, mpaka sasa hicho ndicho anachosimamia.

Kutokana na makubaliano hayo au malengo hayo mawili mpaka sasa Patrick Aussems ameshatimiza moja ambalo ni la kuingia hatua ya makundi, mpaka sasa Simba kwa sasa ipo hatua hiyo ikiwa group D na hilo lilikuwa lengo la klabu hata kama ikitolewa Mbelgiji huyo ametimiza kile alichotakiwa kukifanya.

Aussems pia bado yupo kwenye hatua nzuri ya kutimiza lengo la pili lililobaki ambalo ni kuhakikisha anatetea ubingwa wa ligi kuu walio utwaa msimu wa mwaka 2017/18 Simba ikiwa chini ya kocha Mfaransa, Pierre Lechantre aliyetimuliwa kazi mwezi wa Aprili baada ya kudumu kwa miezi sita pekee.

Image result for kocha wa simba Pierre Lechantre,

Malengo hayo yapili nayo yanaonekana kwenda vizuri kwakuwa nafasi ya nne kwakuwa na pointi 33 ikiwa imecheza michezo 14 huku vinara wa ligi Yanga wakiwa wamecheza mechi 20 na alama 53 hivyo Simba kama itashinda viporo vyake vyote itapishana pointi mbili kwani itakuwa imejikusanyia alama 51.

Kabla ya kutua Simba, Aussems anahistoria ya kuzinoa timu zinazoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa kama ES Toyes AC na Stade de Reims, AC Leopards wakati timu ya mwisho kuifundisha ikiwa ni Napel mwaka msimu wa mwaka 2015/16.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents