Wizkid asema R.Kelly alimpigia simu kumwomba kufanya naye collabo kwaajili ya album yake

Wizkid kutoka Nigeria ambaye tayari yuko jijini Dar kwaajili ya show ya leo (Oct.31), amezungumzia kuhusu mafanikio yaliyoletwa na hit song yake ‘Ojuelegba’ kimataifa.

wizkidayo

Katika mahojiano na East Africa Radio, Wizkid amesema miongoni mwa mafanikio yaliyoletwa na wimbo huo ambao Drake alivutiwa nao na kuamua kufanya Remix, ni pamoja na kumkutanisha na wasanii wengi wakubwa wa kimataifa ambao wamekuwa wakimpigia simu kumwomba kufanya naye kazi.

Wizkid amesema kuwa mfalme wa R&B kutoka Marekani, R.Kelly alimpigia simu na kumuomba wafanye collabo ambayo ni wimbo utakaokuwa kwenye album yake (R.Kelly), so itakuwa ni R.Kelly akimshirikisha Wizkid.

“I just did a record with R.Kelly…it is a record for his album” amesema Wizkid.

Wasanii wengine wakubwa kutoka Marekani ambao Wizkid ameshafanya nao kazi ni pamoja na Chris Brown aliyemshirikisha kwenye wimbo uitwao ‘African Bad Girl’ utakaokuwepo kwenye album yake mpya iliyokuwa itoke mwaka huu, kabla ya kusogezwa hadi mwakani 2015.

Related Articles

Back to top button