Burudani

Wizkid na Davido kuchuana kwenye kipengele kimoja katika ‘BEFFTA UK AWARDS 2014’

Mastaa kutoka Nigeria Wizkid na Davido wametajwa kuwania tuzo za ‘Black Entertainment, Film, Fashion, Television and Arts’ (BEFFTA UK AWARDS 2014) nchini Uingereza.

wizkid-davido2

Davido na mpinzani wake Wizkid wanawania kipengele kimoja cha ‘Best International African Act’, huku wakichuana na wasanii wengine kama Sarkordie, P Square, Timaya, Olamide, Eddy Kenzo na Wande Coal.

Wasanii wengine kwenye kipengele hicho ni Awilo Longomba, Tiwa Savage, Emma Nyra, Burna Boy na Nathalie Makoma.

Wasanii kutoka Afrika Mashariki wanaowania kipengele hicho ni kundi la Saut Sol kutoka Kenya. Jose Chameleone wa Uganda anawania kipengele cha Video Bora ya Muziki kupitia video yake ya ‘Wale Wale’.

Upigaji wa kura umeanza Jumatano October 15 na utasitishwa Jumatano ijayo October 22 na tuzo hizo zitatolewa October 24 & 25 jijini London.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents