Habari

XENOPHOBIA: Kagame na Marais wengine wawili wasusia mkutano wa uchumi wa WEF, Rais wa Ghana atoa somo kwa raia wa Afrika Kusini

Rais wa Rwanda, Paul Kagame hatoweza kuhudhuria mkutano wa uchumi wa WEF ulioanza leo Septemba 4, 2019 nchini Afrika Kusini.

Akieleza sababu za kutoshiriki Rais huyo, Msemaji wa Idara ya kimataifa ya uhusiano na ushirikiano nchini Afrika Kusini (DIRCO), Lunga Ngqengelele, amesema kuwa Kagame hatashiriki mkutano huo na hajajua kama sababu za vurugu za wazawa kuwapiga wageni zinazoendelea nchini humo au laah, Kwani barua ya kutofika kwake haijaeleza sababu.

Marais wengine ambao mpaka sasa hawajatoa taarifa yoyote na hawajatuma muakilishi kwenye mkutano huo wa kimataifa, Ni kutoka Malawi na DR Congo.

Tumepokea taarifa kuwa Kagame hatahudhuria kwenye mkutano wa WEF, Marais wengine ambao mpaka sasa hatujui kama watakuja au laa. Ni Rais wa DR Congo na Malawi. Hao mpaka sasa hawajatuma mwakilishi na hawajatuma barua yoyote ya kutohudhuria kwao.“amesema Lunga Ngqengelele.

Mkutano wa WEF umeanza leo Septemba 4, 2019 na utamaliziki Septemba 6 Jijini Cape Town nchini Afrika Kusini.

Wakati hayo yakijiri, Rais mstaafu wa Ghana, John Mahama ametoa mtazamo na kuwaelimisha wazawa wa Afrika Kusini kuwa Taifa lao isingekuwa mataifa mengine ya bara la Afrika, Ingekuwa inatawaliwa hadi leo.

https://www.instagram.com/p/B1_kZ9KhDdJ/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents