Habari

Simbachawene avifutia mbali vibali vya wafanyabiashara wa vyuma chakavu “Vitolewe upya kuna rushwa kubwa sana” – Video

Simbachawene avifutia mbali vibali vya wafanyabiashara wa vyuma chakavu "Vitolewe upya kuna rushwa kubwa sana" - Video

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, George Simbachawene amemuagiza Katibu Mkuu wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira NEMC kufuta vibali vyote vya zamani vya wafanyabiashara wa vyuma chakavu. Amesema kuundwe tume ambayo itakayosimamia utengenezaji wa vibali vipya vitakavyokidhi matakwa ya kibiashara.

Amesema hayo mapema leo Septemba 4, jijini Dar es salaam wakati anaongea na Wafanyabiashara wa Vyuma chakavu. Simbachawene amesema vibali vyote vilivyotolewa awali vimefutwa na utaratibu wa kuboresha vibali hivyo utafanyika upya ndani ya siku Saba.

Amemwagiza Katibu Mkuu na wenzake waunde kamati ndani ya saa 24 ambayo itatengeneza vibali vipya na wavigawe upya kwa wafanyabiashara na kwa wale ambao walilipia awatalipa tena. “Kamati iundwe ndani ya masaa 24 na iweze kufanya kazi kwa siku saba kukamilisha hivyo vibali vipya”anasema Chawene. Pia aliwataka Nemc kuweza kuwasikiliza wafanyabiashara hao na kuzingatia ukusanyaji wa tozo ili kukuza uchumi wa nchi.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents