HabariMichezo

Yanga, Simba katika ndoto za kuvuka Makundi

Katika mechi za awali timu pekee zilizokuwa zinawakilisha Tanzania ni Yanga SC pamoja na Simba ziliingia na miguu mibaya katika michezo hiyo huku Wananchi wakianza kwa kipigo dhidi ya CR Belouizdad cha Mabao 3-0 wakiwa ugenini.

Tafsiri ya kupoteza mechi hii ilileta presha sana kwa Wachezaji maana mwanzoni kulikuwa na imani kuwa Yanga hatoweza kupoteza ugenini alama zote tatu, wakati huohuo mchezo uliokuwa unafuata ni dhidi ya Bingwa mtetezi AL Ahly ya Misri mechi ilichezwa kwa presha sana kwa Wananchi na kuwafanya kuondoka na alama moja tu ukiwa ni mwendelezo mbaya kwao na kuwafanya waangukie mkiani mwa kundi D wakiwa wana alama moja tu, mpaka kumalizika kwa mzunguko wa kwanza Yanga aliweza kuambulia alama mbili tu baada ya kupata sare dhidi ya Medeama ya Ghana,

Mara baada ya mzunguko wa pili kuanza wakafanikiwa kuwa kwenye nafasi ya pili ya kundi baada ya kumfunga Medeama katika uwanja wa Benjamini Mkapa, kwasasa maombi yote ya Yanga yanaangukia kwenye mchezo wa CR Belouizdad dhidi ya AL Ahly kwa kuombea Mafarao wa Misri waondoke na ushindi ili kuwafanya wao wawe wamebakiza alama 3 tu ili kuingia Robo Fainali.

Simba wakiwa nyumbani pia walianza vibaya mechi za awali baada ya kuambulia sare na ASEC Mimosas ya Ivory Coast 1-1, wakaenda kucheza mchezo mwengine dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana Wekundu wa Msimbazi wakiwa ugenini wakaambulia sare ya 0-0 na mchezo mwengine alienda kucheza dhidi ya Wydad AC ya Morocco na kuambulia kipigo cha bao 1-0 wakiwa nchini Morocco.

Simba ili kufuzu anatakiwa ashinde mchezo mmoja na sare moja huku akiomba mabaya kwa Wydad AC na Jwaneng Galaxy ili yeye aweze kufuzu kufika robo fainali.

Je, Watanzania tunaziona timu zetu zikiwa na njia nyeupe katika kufuzu au nani ananjia ngumu zaidi hapo? Tupe maoni yako.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents