Michezo

Yanga yatwaa ubingwa wa VPL

Klabu ya Yanga imetwaa rasmi ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2015/16 ikiwa ni mara ya pili mfululizo baada ya Simba kufungwa na Mwadui FC katika mchezo wa jana bao 1-0.
????????????????????????????????????

Yanga inatwaa ubingwa kutokana na kuwa na pointi 68 ambazo siyo Simba (yenye pointi 58) wala Azam (iliyofikisha point 60) ambao wataweza kuzifikisha.

Katika mchezo huo, Simba imeonesha kiwango cha juu ambapo licha ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, washambuliaji wake wakiongozwa na Hamis Kiiza walionesha ubutu na kupoteza nafasi nyingi za kufunga.

Bao la Mwadui limepatikana katika kipindi cha pili katika dakika ya 73 kupitia kwa Jamal Mnyate baada ya mabeki wa Simba kuzembea kukaba katika eneo la hatari, na kumpa Mnyate mwanya wa kumchambua kipa wa Simba Vincent Agban.

Katika mchezo huo, mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib ameambulia kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya mchezaji wa Mwadui.

Katika mchezo mwingine, Azam imeichapa Kagera Sugar mabao 2-1 katika uwanja kambarage Shinyanga. Na kufanikiwa kushika nafasi ya pili huku ikiiacha Kagera ikiwa katika hatihati ya kushuka daraja.

Mabao ya Azam yamefungwa na Kipre Tchetche dakika ya 46 na Himid mao dakika ya 59 baada ya Kagera kutangulia kwa bao lililofungwa na Adam Kingwande

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents