Michezo

Yaya Toure akubali yaishe Man City

Kiungo wa kati wa Manchester City amesalimu amri na kumuomba msamaha wasimamizi wa klabu hiyo baada ya kutochezeshwa kwa muda na meneja wa klabu hiyo Pep Guardiola.
yaya-toure-net-worth

Kupitia taarifa kwenye ukurasa wake wa Facebook, amesema: “Naomba radhi – kwa niaba yangu na watu wanaoniwakilisha – wasimamizi wa timu na wote wanaofanya kazi katika klabu hii kwa sababu ya suitafahamu zilizotokea awali.

“Matamshi hayo hayawakilishi msimamo wangu kuhusu klabu au watu wanaofanya kazi katika klabu hii.”

Taarifa ya Yaya Toure

Please see my statement on the situation at Manchester City:

“I wish to apologise – on behalf of myself and those who represent me – to the management team and all those working at the club for the misunderstandings from the past.

“Those statements do not represent my views on the club or the people who work there.

“I have nothing but respect for Manchester City and only wish the best for the football club.

“I am immensely proud to have played a part in the club’s history and want to help City succeed further. I live to play football and entertain the fans.

“On that note, I would like to thank all of the fans for their messages through this difficult period. This means a great deal to me and my family.”

Wiki iliyopita, Guardiola aliambia wanahabari kwamba anamuhitaji Toure lakini bado anasubiri kuombwa msamaha na ajenti wa mchezaji huyo.

Raia huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 33, amecheza mara moja msimu huu, katika Kombe la Klabu Bingwa Ulaya

Baadaye aliwachwa nje katika kinyang’anyiro hicho.

Dimitri Seluk, wakala wa Yaya Toure, alidai mchezaji huyo alikuwa amefedheheshwa na uamuzi huo wa kumuacha nje ya kikosi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents