Burudani

Young Dee ajipanga kuachia mixtape yake

Rapper Young Dee amesema anajipanga kuachia mixtape yake.

Dar

Amedai kuwa yeye na uongozi wake wa MDB wamejadiliana na kuona kuna umuhimu wa kuanza kutoa nyimbo nyingi kwaajili ya mashabiki katika mfumo wa mixtape.

“Nyimbo zipo nyingi sana halafu nilikuwa kimya tulifikiria mwishoni mwa mwaka huu tutengeneze platform ambayo watu wataweza kupata ngoma zangu online, zitakuwa katika mfumo wa mixtape,” rapper huyo alimweleza mtangazaji wa Jembe FM, JJ.

Amesema tayari ameanza kuandaa kazi mpya kwaajili ya mixtape hiyo na baadaye ndipo watatangaza lini itatoka.

Hivi karibuni rapper huyo aliachia wimbo wake ‘Hands Up.’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents