Burudani

Young Killer adai kuchezwa sana redioni sio kipimo cha nyimbo bora

Rapper Young Killer amewataka mashabiki wa muziki kuacha kupima uzuri wa wimbo kwa kuangalia inavyochezwa redioni bali waangalie wakati wa show nyimbo hizo zinapokelewaje na mashabiki.

11380981_1001718373173270_748658765_n

Young Killer ameiambia Bongo5 kuwa katika show yake yoyote silaha yake ni ngoma zake ‘Umebadilika’ na ’13’ ambazo amedai akiimba lazima mashabiki wainuke.

“Hakuna ngoma yangu inakubalika kama Umebadilika.” amesema rapper huyo. “Unajua kipimo kikubwa ni show huwezi ukapima kitu kwa kusikiliza mitaani, imepigwa redioni au wapi. Kipimo kikubwa ni show,” ameongeza.

“Lakini amini usiami hakuna ngoma inayonyanyua mashabiki wa muziki yaani hata kama show ikiwa kidogo imepooza nikipiga hiyo ngoma inanyanyua mashabiki. Hakuna ngoma ambayo ni silaha yangu kama Umebadilika. Umebadilika ni ngoma ambayo inanisaidia sana yaani inanyanyua sana mashabiki ikifuatiwa na 13 ngoma ambazo oya oya sana.”

Katika hatua nyingine Young Killer amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ujio wa kazi yake mpya iitwayo ‘Do 4 me.’

“Do 4 me ni ngoma ambayo haitapooza kama Umebadilika. Hii ni kama Dear Gambe na ndio inamaliziwa mixing na Man Water.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents