Burudani

Zola D na Nazizi kuja na ‘Workout TV Show’

Rapper Zola D na rapper wa kike wa Kenya, Nazizi wanatarajia kuja na kipindi cha TV kiitwacho ‘Workout TV Show’ kitakachohusiana na ufanyaji mazoezi na kitaoneshwa kwenye runinga za nchini Kenya.

Zola Dee

Zola D amesema project hiyo haitomzuia kutoa burudani kwa mashabiki wake kupitia muziki .

“Kwenye muziki bado nipo poa na hivi tayari nina kazi kadhaa na video ambazo nitaachia hivi karibuni, sema nilikuwa busy na maandalizi ya TV Show yetu mimi na Nazizi wa Kenya,” ameiambia Bongo5.

“Lakini kwenye muziki nilikuwa break kidogo kwa sababu hivi karibuni nilikuwa nchini Kenya pamoja na Nazizi kwa ajili ya maandalizi ya show yetu ‘Workout’ ambayo mpaka sasa tayari tumesharekodi episode moja na bado tunaendelea na ikikamilika itaanza kuonyeshwa na TV za Kenya kwa sababu watu wa Kenya wameipenda baada ya kumuona Nazizi amepungua kilo nyingi baada ya kufanya mazoezi,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button