Habari

Facebook inatumia simu za watu kusikiliza wanachozungumza, asema Profesa

Facebook inasikiliza mazungumzo ya watu muda wote, mtalaam wa masuala ya teknolojia ameonya. App hiyo inadaiwa kutumia simu za watu kukusanya taarifa ya kile wanachokizungumza, imedaiwa.

image

Kwa upande wake Facebook inadai kuwa app yake inasikiliza kinachotokea duniani lakini kama njia tu ya kuona nini watu wanasikiiza au kuangalia kwenye tovuti hiyo.

Kitu hicho kimekuwepo kwa miaka sasa lakini onyo la hivi karibuni la Kelli Burns, profesa wa mawasiliano katika chuo kikuu cha South Florida, limetiliwa mkazo.

Profesa Burns amedai kuwa kifaa hicho kinatumia sauti inayoichukua si  kuwasaidia watumiaji, lakini kinaweza kuwa kinafanya hivyo kusikiliza mijadala na kuitunza kwaajili ya matangazo. Amesema kujaribu uwepo wa kitu hicho, alijadiliana mada kadhaa karibu na simu na kisha kugundua kuwa tovuti hiyo imeonekana kuonesha matangazo yanayohusiana na alichokizungumza.

Madai hayo yanaendana na ripoti zilizopo kuwa tovuti hiyo huonesha matangazo ya vitu ambavo watu wamevitaja kwenye mazungumzo yao. Facebook imedai kuwa husikiliza sauti na kukusanya taarifa kutoka kwa watumiaji lakini haitumii sauti hizo kuamua kile kinachoonekana kwenye tovuti.

Kwa sasa kifaa hicho kinapatikana Marekani tu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents