Michezo

Afrika katika World Cup

Bara la Africa hususan nchi ya Afrika ya Kusini inajivunia kuandaa mashindano ya kombe la dunia. Mimi kama Muafrika nahamasika sana kwa hili. Sherehe za ufunguzi zilikuwa za aina yake mjini Johannesburg ambapo mastaa wa ukweli walipamba show hiyo akiwemo R.Kelly, kwaya ya Soweto na wengine wengi. Rais wa nchi hiyo alizungumza kwa niaba ya wananchi na waafrika wa bara zima akitoa shukrani za dhati kwa kamati kamati na uongozi wa Fifa kwa kuchagua kuja Afrika kwa mara ya kwanza.

 

Tukirejea kwenye soka lenyewe ingawa mpaka sasa ni mechi chache zilizo kwisha chezwa ,Wadau wengi wa soka wamekiri bado kutokuona Ladha ya kombe la dunia la 2006. Baadhi ya watazamaji walikpoongea na Bongo5 walisema kuwa bado mapema lakini kombe la 2006 lilionyesha wachezaji stadi zaidi kuliko wengi wanaocheza kombe la dunia mwaka huu.

 

“2006 lilikua na ladha zaidi haswa ukitazama wachezaji walioshiriki fainali hizo kuonyesha uwezo mkubwa kisoka tofauti na sasa.” alisema mdau mmoja huko Mbagala.

Kuna baadhi pia wanaosema soka la kipindi hiki lina msisimuko mkali kutokana na kuwepo kwa wachezaji wakongwe walio shiriki 2006,na kusema kwasasa wamekua na uwezo mkubwa zaidi kisoka kama Wayne Rooney wa Uingereza, Pina wa Bafana Bafana pamoja na Lionel Messi wa Argentina.”Kiwango cha soka kimeonyesha kuwa ni tofauti sana kwani wachezaji hawa wamejinoa vilivyo”.

Ni wachezaji waliojiandaa kutetea mataifa yao. Lionel Messi alionyesha cheche katika mechi dhidi ya Nigeria lakini kutokana na kipa wa Nigeria,Victor Enyeama kuwa makini,mashuti ya Lionel Messi yaliishia mikononi mwa kipa huyo. Kwa upande Wayne Rooney mchezo wake ni kama tulivyomzoea kwa ukali wa mabao.

Kwa upande mwingine, swala la wachezaji nyota kuachwa kwenye vikosi vyao vya Kitaifa kutokana na majeruhi limekuwa tatizo kubwa kwa timu kama ya Bafana Bafana,Ghana na Nigeria,hasa kutokana na kutokua na wachezaji wazoefu wa michuano mikubwa kama hii ya Kombe la Dunia.

Kwa msimu huu timu za bara la Afrika limejikuta kwenye matatizo baada ya wachezaji kama Micheal Essien na Mikel Obi kutokuwepo na kupelekea mataifa yao kuwa kwenye wakati mgumu kwenye mpambano na nchi nyingine.

Kwa timu za Africa zilizokwisha cheza mpaka sasa hivi zimeonyesha uwezo na matarajio makubwa. Ijapokua timu ya Bafana Bafana kutoka sare na Mexico na Nigeria kufungwa goli moja na Argentina na bado tunategemea mengi mazuri kama Ghana kuwa timu ya kwanza kutoka afrika kushinda mechi kwa kuwafunga Serbia goli moja.

Tuzidi kuliombea bara la Afrika kwenye michuano ya WC 2010.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents