Agnes Masogange ni mwanamke kama wanawake wengine – Rammya Gallis

Muigizaji wa filamu Bongo Rammy Gallis ambaye alikuwa akitoka kimapenzi na mrembo Agnes Masogange amefunguka jinsi alivyomchukulia mrembo huo kipindi cha mahusiano yao.

Rammy na Agnes Masogange enzi za mahusiano yao

Akiongea katika kipindi cha Mcheza Kwao -Star TV, Rammy ameeleza kuwa alikuwa akimchukulia mrembo huyo kama wanawake wengine ndio maana akawa naye ila kutokanana tofauti zao ndipo wakaachana.

“Agnes ni msichana kama wasichana wengine tofauti labda ni vile alivyo, sina sehemu ya kuzungumzia jinsi alivyo, labda jinsi anavyoyaweka maisha yake. Ni msichana mzuri kila mwanaume anatamani kuwa naye kuanzisha maisha naye, naamini hakuna mwanaume anayeweza kukata kuwa na mahusiano naye,” amesema Rammy Gallis.

Kwa sasa muigizaji huyo ameadiwa kuwa katika mahusiano na muigizaji kutoka Nigeria, Princess Shyngle.

Na Laila Sued

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW