Promotion

AIRTEL YASAIDIA SHULE ZA SEKONDARI TANGA

Tanga_Airtel_msaada

Yagawa vitabu vyenye  thamani ya shilingi milioni 4 kwa sekondari Old Tanga, Tanga Technical, Toledo na Pande. Mkuu wa Wilaya ya Tanga aishukuru Airtel na kuwasisitiza wanafunzi kujiendeleza kwa manufaa ya jamii na taifa.


Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel  kupitia mpango wake wa Airtel shule yetu imetoa msaawa vitabu vyenye thamani ya shilingi milion nne kwa shule   za sekondani  za mkoani Tanga

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo  Afisa Biashara wa Airtel mkoani Tanga John Nada amesema kampuni ya airtel  kwa kutambua umuhimu wa kuendeleza elimu nchini  inatumia sehemu ya faida inayopata  na kuirudisha kwa watanzania  ili kuboresha huduma za kijamii ambapo hadi sasa imeshatumia zaidi ya shilingi bilion moja kusaidiakuboresha elimu katika nyanja mbalimbali hapa nchini

Shule zinazofaidika na msaada huu hapa mkoni Tanga ni Tanga Technical Sekondari iliyoko Makorora, Old Tanga iliyopo Tanga mjini, Pande sekondari, iliyoko pande njia ya kuelekea Horohoro pamoja na Toledo sekondari iliyoko maeneo Gofu.

Tanga_Airtel_face

Gharama ya vitabu tunavyokabidhi kwa ujumla vinathamani ya shilingi milioni moja kila shule, na vitabu wanavyopata kila shule ni vtabu vya kiada vya English, sayansi, fizikia, na Hesabati, Lengo letu ni kusaidiana na serikali kuinua kiwango cha elimu ya kila mkoa na dio maana tunatoa msaada huu kwenye mikoa yote

Akziungumza wakati wa kupokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Tanga  Dr.Ibrahimu Msengi  aliishukuru airtel pamoja na kuwasisitiza wanafunzi wa shule zote zilizofaidika kuvitumia vitabu kikamilifu ili kujiendeleza kwa manufaa ya jamii zao pamoja na taifa kwa ujumla

  “Msaada  wa Airtel wa Vitabu umekuja wakati  shule nyingi za sekondari mkoani Tanga zikikabiliwa na upungufu wa vitabu, hivyo hii itasaidia wanafunzi katika kupata maarifa zaidi kwenye masomo”

Sasa ni jukumu lenu wanafunzi kutumia fursa hii kusoma kwa bidii ili muweze kusaidia taifa baada ya kisomo chenu, msaada huu mkiutumiavizuri ni nyenzo kubwa sana yakusaidia hata faimilia zenu kutokana na faidakubwa mtakayopata kutokana na zao la elimu” alimaliza kusema Dr. Msemi

Wakipokea msaada huo walimu na wanafunzi wa shule za hizo za sekondari  Old Tanga,Tanga Technical,  Pande na Toledo  wamepongeza mpango wa kampuni ya simu Airtel kuwekeza katika elimu na kuomba makampuni mengine kuona umuhimu wa kusaidia katika sekta ya elimu.

tanga_airtel_msaada_wa_pili

Akiongea kwa Niaba ya walimu wakuu wa shule zilizofaidika na mpango wa Airtel shule yetu Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari  OldTanga  Kavumo Juma Mzirai alisema “ tunawashukuru sana kwa msaada huu wa vitabu ambavyo tunaamini vitatusaidia kuongeza tija katika ufanisi wa kazi zetu pamoja na kusaidia kuboresha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi tunaowafundishia”

Akitoa mfano kuonyesha kiwango cha upungufu ya vifaa vya kufundishia alieleza “Mfano shule ya Old Tanga sekondari inajumla ya wanafunzi wapatao 1,050 ambapo  upungufu wa vitabu  kwa sasa kuna uwiano wakitabu kimoja kwa wanafunzi sita hivyo msaada huu ni dhahiri utapunguza kwakiasi kikubwa tatizo tulilo nalo pamoja na kuturahisishia kazi sisi waalimu

Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia sekta ya elimu kupitia mpango wake wa Airtel Shule Yetu bado inasaidia  shule mbali mbali za sekondari hapa nchini kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo za vifaa vya kufundisha pamoja na ukarabati wa majengo ya shule hizo kwa lengo la kusaidiana na serikali kutimiza dhamira ya kuinua kiwango cha elimu kila mahali.

Mwisho

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents