Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Askari wawili wa JWTZ wauwawa nchini DRC

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limetangaza vifo vya Askari wake wawili Koplo Maselino Paschal Fabusi na Praiveti Venance Moses Chimboni, ambao walikuwa katika Ulinzi wa Amani nchini DRC.

Askari hao wamefariki baada ya kushambuliwa kwa kupigwa risasi na kundi la waasi tukio ambalo limetokea tarehe 9, Oktoba mwaka huu umbali wa kilomita 24 Mashariki mwa mji wa Beni. Majeshi yetu yamefanikiwa kuwarudisha nyuma waasi hao na kudhibiti eneo hilo.

Kufuatia shambulizi hilo Umoja wa Mataifa umeunda Bodi ya Uchunguzi kuchunguza tukio hilo. Aidha, Maafisa na Askari wa JWTZ wanaendelea kutekeleza majukumu yao katika Operesheni hiyo.

Umoja wa Mataifa unaandaa utaratibu wa kuleta miili ya marehemu nchini. Hivyo taarifa za mapokezi kuiaga miili hiyo itatolewa.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW