Tupo Nawe

Aslay aendelea kuwa mwiba kwa wasanii wakubwa

Msanii wa muziki, Aslay wiki hii ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Kwatu’ ambao umeonekana kukubalika zaidi na watu kwa muda mfupi.

Muimbaji huyo toka aachane na Yamoto Band mwaka mmoja uliopita na kuanza safari yake mpya ya muziki akiwa binafsi hakuwahi kupoa au kutoa ngoma ambayo haijafanya vizuri.

Kwatu ni moja kati ya ngoma kali ambazo zimeachiwa wiki hii, nyingine ni Iokote ya Mausa Sana na Hanstone, Zaidi ya Jux, Kudamshi wa Dully Syke akiwa na Harmoniza, Why ya Ben Pol na Harmonize pamoja na Mpaka Naogopa ya Z Anto.

Kwa sasa Aslay ni mmoja kati ya wasanii wa muziki ambao wanaangalia kwa jicho la pekee kutokana na kuachia ngoma nyingi kali mfulizo.

Muimbaji huyo tayari ameshaanza kushindanishwa na wasanii kama Diamond, Rayvanny, Harmonize pamoja na wengine wengi.

Huwenda moto huo aliouwasha ukawa ni mwiba kwa wasanii wengi kwani tunajua namna tasnia ya muziki ilivyokuwa na ushindani kwa sasa kila msanii anataka kuwa juu ya mwenzake.

Kama muimbaji huyo ataendelea hivyo, basi atafika mbali zaidi na kuwapita kimafanikio wasanii wengi wakubwa ambao bado wanajikongoja.

https://www.youtube.com/watch?v=ykul-DHwD6g

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW