Michezo

Australian Open 2018: Roger Federer amtupa nje mbabe wa Nadal, atinga fainali kwa kishindo

Bingwa wa mchezo wa tenisi duniani Roger Federer amefanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ya michuano ya Australian Open 2018.

Federer ambaye anashika namba moja katika viwango vya ubora wa mchezo huo dunian, ametinga katika hatua hiyo baada ya kumtupa nje Chung Hyeon, 21, kwa seti 6-1 5-2.

Mchezo huo ulichezwa kwa muda wa dakika 63 pekee kutokana na Hyeon kupata majeraha ya mguu wake wa kushoto ambapo alishindwa kuendelea na mchezo huo na kuamua kujitoa.

Kutokana na ushindi huo wa Roger Federer atakutana na Marin Cilic kutoka Croatia katika mchezo wa fainali ambao utapigwa Jumapili ya January 28, mwaka huu.

Endapo Federer atafanikiwa kushinda fainali hiyo litakuwa ni taji lake la sita katika mashindano hayo na taji lake la 20 katika mashindano yake yote makubwa tangu alipoanza kucheza mwaka 1998.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents