Tia Kitu. Pata Vituuz!

Baada ya kujeruhiwa ‘Mnyama’ Simba afanya mauaji ya kikatili Singida, Mo ashindwa kujizuia (+Video)

Mabingwa wa tetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba Sports Club wamefanya mauaji ya kutisha mbele ya Singida United katika mchezo wa ligi kuu kwa mabao 8 – 0.

Simba hii leo haikuwa na muda wa kupoteza mbele ya mpinzani wake Singida baada ya kuanza kufunga magoli sita (6) katika dakika 42 pekee za kipindi cha kwanza hata kabla ya mapumziko.

Na kipindi cha pili kumalizia mawili hivyo kufikisha magoli 8- 0. Wafungaji hii leo alikuwa ni Medie Kagere akifunga manne (4), Deo Kanda mawili (2) na John Bocco mawili (2).

Mara baada ya ushindi huo Bosi wa klabu hiyo, Mo Dewji ameonyesha furaha yake kwa kuposti kipande cha video kwenye akaunti yake ya Instagram kinachomuonesha akicheza na dada mmoja mwenye asilia ya asia huku akiandika ujumbe ”Mwenyezi Mungu atusimamie tuendelee kufanya vizuri na kupambana kwa mwendo huu!”

Wiki iliyopita Simba iliambulia kipigo cha goli 1 – 0 kutoka kwa mtani wake wa jadi Yanga mchezo uliyoibua maneno mengi mtaani hasa kutoka kwa masahabiki wa hasimu wao wa Jangwani.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW