Michezo

Barcelona yatoa taarifa hii kuhusu Dembélé

Winga wa Barcelona, Ousmane Dembélé ametajwa kukaribia kujiunga tena na mabingwa hao wa La Liga baada ya kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu akiuguza majeraha.

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo umethibitisha hilo baada ya mchezaji huyo kuonekana kupona majeraha yake ya mguu wa kushoto aliyoyapata wakati wa mchezo wao dhidi ya Getafe Septemba 16.

“Kurudi kwa Ousmane Dembélé uwanjani kunakaribia. Kwa kweli, Jumanne hii alipata matibabu kutoka kwa Huduma za Kliniki za Klabu na, kwa hiyo, Ernesto Valverde anaweza kumtumia. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 atakuwa na uwezo wa kucheza tena, miezi mitatu na nusu baada ya kupasuka kwa tendon ya biceps ya mguu wake wa kushoto, majeruhi yaliyotokea dhidi ya Getafe mnamo Septemba 16,” umesema mtandao huo.

“Licha ya haja ya kufanyiwa operesheni nchini Finland, Dembélé haraka alianza mchakato wake wa kurejesha na kuanza kufanya kazi yake Ciutat Esportiva mnamo Disemba 6, kumalizika Januari 2. Kabla ya kuumia, alicheza dhidi ya Espanyol na Juventus katika michezo yake ya kwanza akiwa na Barcelona, assist yake ya kwanza ilikuwa kwa Suárez,” umeongeza.

Ousmane Dembélé alisajiliwa na Barca msimu huu akitokea Borussia Dortmund kwa dau la paundi milioni 105.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents