Michezo

Barcelona yawapiga ‘stop’ mashabiki wake

Klabu ya soka ya FC Barcelona inayoshiriki Ligi Kuu nchini Hispania ‘La Liga’ imesema haitasafiri na mashabiki wake kwenye mchezo wao dhidi ya Atletico Madrid wiki ijayo utakao pigwa kwenye dimba la Wanda Metropolitano Jijini Madrid.

 

Uongozi wa Barcelona umetuma taarifa kwa viongozi wa Atletico Madrid ukiwataka wasiuze tiketi kwaajili yamashabiki wa timu hiyo bali wafanye hivyo kwaajili ya mashabiki wao pekee.

Barcelona imefikia uamuzi huo kufuatia vuguvugu lililopo nchini Hispania ambapo Wananchi wa Jimbo la Catalonia yalipo makao makuu ya klabu hiyo wamepiga kura ya kujitenga kutoka nchi ya Hispania.

Mechi iliyopita ya Barcelona dhidi ya Las Palmas wakiwa nyumbani Camp Nou timu hiyo ilicheza bila mashabiki kwa kuhofia vurugu ambazo zingeweza kufanywa na mashabiki.

Uongozi wa Barcelona umeamua kufanya hivyo ili kuepusha vurugu ambazo huenda zikatokea wakati wa mchezo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents