Videos

[Video] Bi Cheka akichana live! Atakwepo katika tamasha la Pasaka

[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=ddJTT0L6hR4[/youtube] Mwanamuziki Mzee kuliko wote katika muziki wa kizazi kipya, Bi Cheka anatarajia kupanda stejini kwa mara ya kwanza katika tamasha la Pasaka litakalo fanyika mkoani Morogoro.

Bibi Cheka alisema anaitamani sana siku hiyo ya tarehe 8, kwakuwa anahitaji kuonyesha uwezo wake wa kuimba wimbo wa Ni wewe alioshirikiana na Mh Temba.

Aidha Bi Cheka alidai kwamba siku ya Media Day, alipanda kama kujionyesha kwakuwa alishafika kwenye tukio, lakini kwenye tamasha la Pasaka, kwake ndiyo linakuwa tamasha lake la kwanza rasmi.

Katika Tamasha hilo, ambalo litaongozwa na Mh Temba, huku akiambatana na Dogo Muu, Dogo Aslay, Ferooz, Shilole, Ize Man, Nuldin, Mugogo huku wakitetemeshwa na Khanga moko.

Pia mwanamuziki ambaye mdogo wa Aslay atakayekuja kufunika siku za baadaye kwa nyimbo yake ya Shahidi, Dogo Muu atatoa zawadi kwa mtoto ambaye ataperfom vizuri wimbo wa Naenda kusema wa Dogo Aslay.

Watoto watakuwa na nafasi nzuri ya kujishindia zawadi ya Tv nchi 21 atakayeimba Naenda kusema, zawadi zingine ni Mpira, Baiskeli,na begi likiwa full na madaftari yake.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents