Michezo

Bilionea wa Nigeria Aliko Dangote atoa sababu za kutaka kuinunua timu ya Arsenal

Tajiri namba moja Afrika, Aliko Dangote wa Nigeria ametoa sababu za kutaka kuinunua timu ya soka ya Arsenal.

Dangote-OnoBello

Baada ya kutangaza nia yake hiyo amekosolewa na Wanigeria wengi, wakisisitiza kuwa pesa anazotaka kuinunua timu hiyo angenunua timu za Nigeria na kupromote ligi ya ndani kuliko kuzitumia kwa timu ya nje.

Dangote,58 ametoa sababu za uamuzi wake wa kutaka kuimiliki timu hiyo alipozungumza na waandishi wa habari Jumaosi iliyopita jijini Lagos.

“Swala ni kwamba kama nikinunua timu zote za Nigeria, bendera ya Nigeria itaendelea kubaki hapa.Lakini nikinunua Arsenal itaipeleka bendera ya Nigeria dunia nzima. Ni kama kila Abramovich anapotajwa, jina la nchi yake Urusi pia linajitokeza, kila mmoja anafahamu kuwa ni mrusi.” alisema Dangote.

Hii ni mara ya pili Dangote kuonesha nia ya kutaka kuinunua timu ya Arsenal, baada ya kushindwa kufanya hivyo mwaka 2010.

Source: Forbes

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents