Burudani ya Michezo Live

CAF nayo haipo nyuma, wapata taarifa za Ubingwa wa Mnyama Simba

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeipongeza klabu ya Simba kwa kufanikiwa kutawazwa kuwa mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Kupitia akaunti yao ya Twitter, CAF ameandika ujumbe wa kuipongeza Simba SC ”Hongera Simba SC Tanzania.”

Timu ya Simba SC imefanikiwa kutetea taji lake la ubingwa wa Ligi Kuu Tanznaia Bara (VPL) ikiwa bado na mechi sita mkononi baada ya kutoka suluhu na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa leo na kufikisha pointi 79 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye msimamo wa ligi. .

Huu ni ubingwa wa tatu mfululizo kwa Simba baada ya kufanya hivyo pia katika misimu miwili iliyopita 2017/18 na 2018/19. .

Huu ni ubingwa wa tatu mfululizo kwa #simbasc baada ya kufanya hivyo pia katika misimu miwili iliyopita 2017/18 na 2018/19. .

Mnyama #simbasc anafanikiwa kulitetea taji la Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kutoka sare tasa ( 0 – 0 ) mbele ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mtanange uliofanyika Dimba la Sokoine.

SIMBA SC BINGWA KWA MARA YA TATU MFULULIZO
2017/2018 🏆🏅🏅
2018/2019 🏆🏅🏅
2019/2020 🏆🏅🏅

Kikosi hiko cha Mbelgiji, Sven Vandenbroeck wamefikisha pointi 79 baada ya sare ya leo katika michezo 32 ikijihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu, kwani hakuna timu inayoweza tena kufikia alama hizo.

Linakuwa taji la 21 katika historia ya klabu hiyo baada ya awali kulibeba katika miaka ya 1972, 1973, 1976, 1977, 1978, 1979, 1980, 1984, 1990, 1994, 1995, 2001, 2003, 2004, 2007, 2010, 2012, 2018, 2019 na 2020.

Licha ya taji hilo bado Simba itakuwa na mlima mrefu kama wanahitaji kuwafikia watani wao kwenye kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwani Yanga tayari wanamataji 27 baada ya kushinda miaka ya 1968, 1969, 1970, 1971, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992, 1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2008, 2009, 2011, 2013, 2015, 2016 na 2017.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW