Burudani

Cassper Nyovest apanga kujaza ukumbi unaochukua watu 20,000 Oct 1

October 31, rapper wa Afrika Kusini, Cassper Nyovest amepania kuweka historia ya kwanza jijini Johannesburg.

cass

Rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Refiloe Maele atafanya show yake kwenye ukumbi wa Ticketpro Dome unaochukua watu 20,000 kuthibitisha kuwa msanii wa nyumbani anaweza kuujaza.

Lengo ni kuujaza ukumbi huo kuonesha uzalendo kwa kile anachodai kuwa wasouth hawaviungi mkono vipaji vyao kama wafanyavyo kwa wasanii wa Marekani. Amesema anatarajia kufanya show yake mwenyewe ya masaa mawili.

Kama akiweza kuujaza ukumbi huo, atakuwa rapper wa kwanza wa Afrika Kusini kufanya hivyo. Show hiyo ameigharamia yeye mwenyewe ambayo itamcost takriban Rand milioni moja ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 158.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents