Moto Hauzimwi

Chelsea yapata kipigo cha ‘Mbwa Mwizi’ ligi kuu

Ligi kuu ya Uingereza imeendelea tena usiku wa jana (Jumatatu) kwa kucezwa mchezo mmoja, ambapo Watford waliwakaribisha Chlsea katika uwanja wa Vicarage Road ambao unauwezo wa kuchukua watu 21,577.

Katika mchezo huo Chelsea ambao wanashika nafasi ya nne katika ligi hiyo, waliambulia kipigo cha ‘Mbwa Mwizi’ cha magogoli 4-1 kutoka kwa Watford.

Magoli ya Watford yalifungwa na kepteni wao Troy Deeney dakika ya 42 kwa njia ya penati, Daryl Janmaat dakika ya 84, Gerard Deulofeu aliyefunga dakika ya 88, na Roberto Pereyra alihitimisha kwa kufunga goli la nne dakika ya 90.

Nao Chelsea walipata bao lao la kufutia machozi kupitia kwa Eden Hazard dakika ya 82. Wakati huo huo, kwenye dakika ya 30 Tiémoué Bakayoko wa Chelsea alipewa kadi nyekundu na kutoka nje ya uwanja.

Mpaka sasa timu zote za ligi ya Uingereza zimeshacheza mechi 26, na Manchester City anaongoza kwa kuwa na alama 69 wakifuatiwa na Manchester Unitd wenye alama 56.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW