Diamond Platnumz

Diamond aipiga chini tour ya Europe baada ya promoter kushindwa kumlipa

Diamond amelazimika kuipiga chini tour yake ya barani Ulaya iliyokuanza ianze kwa show moja leo March 9 jijini Stuttgart nchini Ujerumani.

diamond-stuttgart-vz copy (1)

Taarifa hiyo imetolewa na Diamond kupitia website yake.

“Kutokana na kampuni ya United Events Ltd Tilburg-The Netherlands kwa upande mwingine kama promoter kushindwa
kutimiza baadhi ya mahitaji ikiwemo kushindwa kulipa pesa ya show ambayo ilitakiwa ifanyike Jugenhause Ostend mjini Stuttgart/Germany 09/03/2013 na zingine kama East African Night ambayo ilitakiwa ifanyike mjini Rotterdam/Holland tarehe 15/03/2013 na kadhalika, mimi na team yangu nzima ya wasafi hatutoweza kuhudhuria kwenye events hizo,” amesema diamond kwenye maelezo yake.

“Nilikuwa nikipata Maswali mengi sana toka kwa mashabiki zangu mbalimbali wakiniuliza kuhusiana na ujio wangu wa nchi hizo za EUROPE lakini siku zote nilikua kimya sikuweza kujibu wala kuzungumza chochote na Wadau wangu kutokana na kutokuwa na uhakika wa tour hiyo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents