Diamond Platnumz

Diamond asema sababu ya kuchelewa kupanda stejini Mombasa ni promoter kushindwa kummalizia hela yake

Wiki iliyopita Diamond Platnumz alisababisha timbwili zito mjini Mombasa baada ya kuchelewa kupanda kwenye steji ya show yake na kusababisha mashabiki kuanza kurusha chupa.

http://www.youtube.com/watch?v=5lrkTZfLH88

Kupitia kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen, Diamond amefunguka kuhusu sababu ya yeye kuchelewa kupanda stejini.

“Nililipwa pesa nusu, nikawa natakiwa nikifika Nairobi nimaliziwe pesa yangu yote iliyobaki lakini baada ya kufika Nairobi nikafanya show nikapewa pesa tena nusu iliyobaki sikupewa,” amesema Diamond.

“So kufika Mombasa nikasema siwezi kupanda kwenye stage mpaka nimaliziwe pesa yangu sio, kwasababu ilikuwa imebaki kama dola elfu sita na kitu, saba kasoro hivi. Nikasema mpaka nimaliziwe pesa yangu ndio nipande kwenye stage. Sababu kulikuwa na uongo uongo kidogo, ‘ukishuka utapewa’ unajua sisi wasanii tulishadhulumiwaga sana, mtu huwezi kumwamini kwamba upande stejini halafu ushuke, lazima upewe chako.

Nikasema ‘mimi nataka mnilipe hela yangu ndio nipande kwenye stage’. Halafu wakati huo show imejaa, sijawahi kuona show iliyojaa hivyo. So baada ya kukamilishiwa pesa yangu ndio nikatoka nikaenda stejini saa tisa hiyo na kitu. Before kabla sijafika watu walikuwa wameshaanza kufanya vurugu, watu walipiga machupa nasikia, vurugu kinomanoma. Lakini namshukuru mwenyezi Mungu nilipofika mimi zile jaziba zote zikapungua watu walikuwa na mizuka.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents