Diamond Platnumz

Diamond ashindwa kutamba kwenye tuzo za MTV MAMA, Davido na Mafikizolo wapeta

Haikuwa bahati kwa Diamond Platnumz na Watanzania Jumamosi hii kwenye tuzo za MTV MAMA, baada ya Diamond Platnumz kuondoka mikono mitupu kwenye tuzo za MTV MAMA zilizofanyika jijini Durban, Afrika Kusini.

4K0A0645
Diamond na Wema kwenye red carpet ya MTV MAMA

Diamond ambaye pia alitumbuiza wimbo wake ‘My Number One’ remix akiwa na Davido, alikuwa ametajwa kuwania vipengele viwili ambavyo ni pamoja na muimbaji bora wa kiume na wimbo bora wa kushirikiana.
Davido, Mafikozolo, Uhuru na Clarence Peters ndio walikuwa washindi wa juu kwenye tuzo hizo.

Wasanii wengine waliotumbuiza ni pamoja na Fally Ipupa, Michael Lowman, Don Jazzy, DJ Clock, Beatenberg, DJ Kent, Big Nuz, Toofan, D’Banj, DJ Vigi, DJ Tira, DJ Buckz, Burna Boy, Sauti Sol, Ice Prince, Sarkodie, The Arrows, Khuli Chana, Dr Sid, French Montana, Miguel, Trey Songz, , Uhuru, Mafikizolo, Oskido, Professor, Tiwa Savage, Flavour na Phyno.

Katika vipengele vipya vya tuzo hizo, muigizaji wa Kenya Lupita Nyong’o alishinda Personality of the Year, wakati ile ya MTV Base Leadership award ikienda kwa mjasiriamali wa Tanzania Ashish J. Thakkar.
Tuzo hizo zilishereheshwa na muigizaji wa Marekani Marlon Wayans.

THE WINNERS OF THE 2014 MTV AFRICA MUSIC AWARDS:

Best Male: Davido (Nigeria)

Best Female: Tiwa Savage (Nigeria)

Best Group: Mafikizolo (South Africa)

Best New Act: Stanley Enow (Cameroon)

Best Live Act: Flavour (Nigeria)

Best Collaboration: “Y-tjukutja” – Uhuru Ft. Oskido, DJ Bucks, Professor and Yuri Da
Cunha (South Africa/Angola)

Best Hip Hop: Sarkodie (Ghana)

Best Alternative: Gangs of Ballet (South Africa)

Best Francophone: Toofan (Togo)

Best Lusophone: Anselmo Ralph (Angola)

Artist of the Year: Davido (Nigeria)

Song of the Year: “Khona” – Mafikizolo ft Uhuru (South Africa)

Best Video: Clarence Peters (Nigeria)

Best Pop: Goldfish (South Africa)

Best International: Pharrell

Personality of the Year: Lupita Nyong’o (Kenya)

MTV Base Leadership Award: Ashish J. Thakkar (Tanzania)

Transform Today Award by Absolut: Clarence Peters (Nigeria)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents