Bongo5 ExclusivesMahojiano

Exclusive Interview: Steve RnB akiizungumzia ‘Jambo Jambo’ na jinsi ilivyompa heshima na mashavu!

Siku za hivi karibuni ni vigumu kupita siku bila kuusikia wimbo wa reggae wa Steve RnB, Jambo Jambo ambao umetokea kupendwa sana nchini. Bongo5 imechat na Steve ambaye kwa sasa yupo barani Ulaya kuhusiana na jinsi alivyopata idea ya kufanya wimbo huo na namna ulivyompa heshima.

Bongo5: Wazo la kufanya Jambo Jambo lilikujaje hasa ukizingatia riddim si maarufu sana Tanzania?

Steve: Kwanza Sweat Reggae ni type ya music ambayo naipenda tuseme ni chaguo la pili baada ya RnB, so wazo lilikuja baada ya kuona wasanii wengi wa Bongo waoga sana kufanya aina hii ya muziki huu wa reggae kama ilivyokua kwenye RnB. So kimya changu kikubwa kilinifanya nifikirie na nikaja na idea ya kufanya riddim. Isitoshe pia style ya artist wengi wa Jamaica wanaitumia , beat moja wasanii tofauti. Niliipenda na ilikuwa inaonyesha uwezo wa kila mtu na kipaji pia cha kuweza kutumia melody mbalimbali, so na mimi nikaona nijaribu kufanya.

Bongo5: Baada ya kuachia audio na video ulitegemea ingeshika hivi?

Steve: Yah nilitegemea ingeshika coz uwezo niliouonyesha humo ni wa kimataifa nadhani hata wewe mwenyewe unaona si kibongobongo kama unavyoona ngoma zingine, this is classic music popote itasikilizwa na kueleweka nini kimefanywa humo ndani.

Bongo5: Mpaka sasa umeshapata mashavu yoyote kutokana na Jambo Jambo?

Steve:
Yah mashavu ni mengi sana ila kwa sasa muda ndio unaonibana coz niko katika tour Europe kwa muda kidogo hopefully after this tour nitarudi nyumbani na kufanya shows mbali mbali nitawafikia tu wapenzi na washabiki wangu, nataka kuwaambia hata Mimi nawa-Miss sana.

Bongo5: Una mpango wa kufanya jitihada iwafikie madj wa Jamaica ili ujiongezee mashabiki huko?

Steve: Tayari tupo kwenye mipango mingi tu ya kuisukuma Jambo Jambo mbele, kwanza kabisa sasa hivi miziki yangu yote inapatikana kwenye itunes, pia tushatuma kwenye studio mbalimbali ikiwezekana iingie kwenye mixtapes tofauti tuweze kusonga mbele. Hili linasimamiwa zaidi na Management yangu Kvelli Entertainment.

Bongo5: Kwakuwa umeonesha kukubalika sana kwenye uimbaji wa reggae ya kisasa ambayo imechanganyika sana na rnb, una mpango wa kuendelea kutoa ngoma nyingi za aina hiyo?

Steve: Kwanza nataka nikuambie kuwa nina nyimbo nyingi tu za dizain hii na nitazitoa kwa kipindi maalum. Unajua sasa hivi kila kitu kinafanyika chini ya maamuzi ya management yangu, kwa mfumo huo huo wa riddim, lakini zaidi nita stick sana kwenye rnb.

Bongo5: Tufahamishe kama una jambo lolote jipya

Steve: Mashabiki wakae tayari kwa surprise toka kwa Steve rnb on 12.2.2013, na mengi mazuri yatawafikia chini ya usimamizi mpya wa Kvelli entertainment.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents