Burudani ya Michezo Live

Exclusive Video: Janjaro aelezea mgongano ulioisha kati yake na Ostaz Juma, Tip Top, na masomo

Rapper wa Arusha, Dogo Janja aka Janjaro amefunguka mengi kwenye interview na Bongo5 kuhusiana na mgogoro wa hivi karibuni na Mkurugenzi wa kampuni ya Mtanashati Entertainment, Ostaz Juma ambaye alikaribia kumuondoa lakini wakafanikiwa kuyamaliza.

Akizungumzia sababu za ugomvi huo, Janjaro amesema: Hakikuwa kitu kikubwa cha kihivyo,ilikuwa ni misunderstanding ambazo zilikuwa zimetokea lakini ziliweza kukaa sawa kwasababu unajua hata glass hugongana halafu kila mmoja ana mapungufu yake. Kwahiyo inabidi sometimes tufiche mapungufu ya mtu ili kuweza kusogea mbele. Tukilumbana hatutafika bora tukae tuyajenge na tumeyajenga. Tuko pamoja na tunapiga kazi wala hakuna kitu kibaya chochote ambacho kinaendelea.


Kuhusu kama kweli anavuta bangi na kulala nje ya sehemu unayoishi

Situmii kilevi cha aina yoyote. Mimi naswali, mimi sasa hivi naishi mwenyewe nimepanga, naishi kwangu lakini bado nipo chini ya Ostaz sio kwamba kuondoka nyumbani ndio mimi sipo na Ostaz. lakini najua mtoto kuna stage inafika anaanza kujitegemea awe na maisha yake, awe na vitu vyake. Kwahiyo huu ndiy muda wa kujenga maisha yangu.


Kuhusu kichonakuja kutoka kwake baada ya Serebuka

Nangoma ambayo nafanya kwa Pancho Latino,nimeshachukua mdundo na nishaandika verse moja namalizia verse moja/. Kwaasababu mdundo wenyewe nimechukua juzi, namaliza ngoma na rekodi. Lakini ngoma hii nitafanya na mwanamke, unajua sijawaHi kufanya ngoma na mwanamke lakini nitafanya ngoma hii na demu yeyote yule na demu huyo hajawahi sikika popote kwahiyo nataka nifanye kitu cha utotauti kidogo na mimetanua upeo wangu wa uandishi nitafanya kitu kizuri.

Kuhusu tofauti iliyopo katika usimamizi na utendaji wa kazi kati Tip Top Connection na alipo sasa Mtanashati

Nachoweza kushukuru kwamba Tip Top walinisimamia vizuri ndio maana Tanzania wakanielewa,saluti kwanza kwa Babu Tale,Madee na Tip Top. Unajua watu wamesha kremu kwamba mtu akitoka Tip Top huwa anapotea katika muziki,lakini nachoweza kushukuru Mungu nimeweza ‘kumentain’ status yangu mpaka hapa nilipo. Tofauti na sasa hivi ukisema ukimtaja msanii aliyotoka Tip Top ukimtoa Cassim,wale wote waliotoka Tip Top yaani hakuna aliyevuma. Kwahiyo nimejitaidi ‘kumaintan’ Ostaz ananisimamia fresh.

Kuhusu fani atakayofanya akimaliza elimu yako ya sekondari

Nikimaliza, tuombe uzima nikimaliza mtihani wa Form 4, O-level nadhani nitaenda chuo, nikienda chuo nitasoma IT,nikisoma IT najua ni kitu ambacho baadaye kitakuwa kitu ambacho kila mtu anakigombania bora nikitafute mapema. Unajua afadhali yule anayeingia ofisini akapata mia 300, kuliko anayekaba apate elfu 10,000.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW