Technology

Fahamu ‘Programu’ inayojizoelea umaarufu mkubwa kipindi hiki cha ‘CORONA’, watu wakutana huko na kufanya vikao

Zoom Video Communications ni programu ya kuwasiliana kupitia video ambapo unaweza kuendesha mkutano, kikao hata mijadala huku mkiwa mnaonana licha ya kila mmoja kuwa mbali na eneo hilo, na Makao Makuu ya Kampuni hii yakiwa San Jose, California.

How Zoom Employees use Zoom

Mikutano hiyo ambayo inafanyika kwa njia ya video unaweza kutumia simu janja za mkononi (SmartPhone), ama Kompyuta katika kuendesha vikao (online meetings) huku zikiunganishwa na ‘Internet’, programu ambayo inakuwezesha pia kuchati.

Man talking via Zoom

Mfumo huu wa ‘ZOOM’ umezidi kuwa maarufu kwa hivi sasa duniani, watu wakizidi kupakuwa ‘App’ yake kutokana na kuwa katika kizuizi ‘Karantin’ cha kutotoka majumbani wakati huu wa mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.

Kwa sasa mamilioni ya watu duniani wamekuwa wakitumia Zoom huku ikiwa kama sehemu salama ya kuktana na kufanya mikutano wakiwa pamoja.

Wiki hii Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson aliposti picha ikimuonyesha akiendesha kikao kupitia mfumo huo wa Zoom.

Hii ni ishara tosha kuwa mfumo huo kwa namna gani ulivyokuwa wa usalama zaidi kwa kukutana na kuendesha mikutano.

Zoom na baadhi ya mitandao mingine ya kijamii ambayo inatumia mfumo wa video imezidi kuwa na thamani kipindi hiki cha mlipuko wa janga la Corona, lakini watumiaji wanapaswa kuwa makini katika machaguo ya matumizi katika kuhakikisha wanalinda haki zao binafsi za mawasiliano ili kutofahamika na watu wengine.

ZOOM IMETOKEWA WAPI ?

Zoom ni jina ambalo limekuwa likipata umaarufu kila mwaka, wakati likijadiliwa kwenye soko la hisa mwaka jana lilikuwa na thamani ya dola za Kimarekani Bilioni 15 (£12bn) lakini sasa imekuwa zaidi hadi kufikia dola za Kimarekani Bilioni 38.5.

Eric Yuan

Eric Yuan muanzilishi wa Zoom na kuiuza kwa Cisco Systems

Zoom ilianzishwa mwaka 2011 na Engineer wa Kichina bwana, Eric Yuan ambaye baadae alihamia  Silicon Valley akiwa na umri wa miaka 27. Kwa sasa  Zoom imekuwa kimbilio kubwa kwa watu kipindi hiki cha mlipuko wa Corona na kuwazidi wapinzani wake sokoni Skype na Microsoft kutokana na kuwa na ‘features’ rahisi katika matumizi.

Mfumo huu wa Zoom ni rahisi mno katika kutumia na pindi unapokuwa kwenye matumizi unapewa kikomo cha muda wa dakika 40 kwa washiriki zaidi ya watatu. Umekuwa ukitumika na waalimu kufundishia wanafunzi katika shule za Uingereza, Canada na Ujerumani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents