AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Filamu ya ‘Tatu Chafu’ kutua mtaani kwako kwa style hii

Filamu ya Tatu Chafu inataraji kuteka viunga vya Dar es salaam pale itakapoonyeshwa kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa burudani Dar Live uliopo mitaa ya Mbagala siku ya Jumamosi tarehe 16. December.2017 kuanzia mida ya saa nne asubuhi huku michezo ya watoto wakicheza michezo mbalimbali kabla ya movie kuruka.

Akiongea na Filamu Central muongozaji wa filamu hiyo Novatus Mugurusi Rrah C amesema kuwa wanasongea karibu na wapenzi wa filamu walipo kwa kuwapelekea sinema nzuri jirani na wao ili wapate nafasi ya kuweza kuiangalia na kuburudika walipo nan kampeni ya nchi nzima kupitia filamu ya Tatu chafu.

Kuna matukio mengi yamepangwa kufanyika na kiingilio ni 5,000/tu utaweza kuona filamu burudani kutoka kwa wasanii wa hip hop kama Wakazi, Mapacha ambao pia ni moja kati ya wasanii walioshiriki katika sinema hiyo, wasanii wakali wa muziki wa Singeli watatumbuiza huku vyakula vinywaji vya uhakika vikiwepo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW