Tupo Nawe

Glory of Ramadhan ya Ray Kigosi sokoni mwezi ujao

Filamu mpya ya muigizaji maarufu nchini Tanzania, Raymond Kigosi iitwayo ‘Glory of Ramadhan’, inatarajiwa kuingia sokoni mwezi ujao, August 6.
Taarifa hiyo imetolewa na yeye mwenyewe Ray kupitia website yake.
“Mzigo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na wadau wa tasnia ya movie bongo sasa unaingia mtaani tarehe sita mwezi ujao ni bonge la movie na wala si yakuikosa maana imejaa mafunzo ya kutosha kuhusu mwezi mtukufu wa Ramadhan.
“Hii filamu inahusu mwezi mtukufu wa Ramadhan lakini ndani yake ina mafunzo mbalimbali hivyo nawaomba mashabiki kuinunua na kuiangalia,” alisema Ray.
Waigizaji wengine walioshiriki kwenye filamu hiyo ni pamoja na Chuchu Hans, Neshi Mohammed ‘Batuli’ , Abdallah Khamis ‘Dulla’ ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na EATV na wengineo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW