Hawa ni washambuliaji 7 wanaomuumiza kichwa Hodgson kwenda UERO 2016
Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson anaelekea kuwa na wakati mgumu kuchagua washambuliaji watakaoisaidia timu hiyo kwenye michuano ya Uero mwaka huu nchini Ufaransa.
Mpaka sasa Hodgson ana chaguo la wachezaji saba ambapo anatakiwa achague wachezaji wanne au watano kati yao.
Hawa ni washambuliaji wanaomuumiza kichwa Hodgson kufanya uchaguzi yupi atakayeshiriki michuano ya Uero 2016.
Harry Kane
Kane ndiyo mchezaji anayeongoza kwa ufungaji kwenye ligi ya Uingereza akiwa ameshafunga magoli 24. Mpaka sasa anaonekana kuingia kwenye orodha ya wachezaji wanaoweza wateuliwa na Hodgson kwenye timu ya Uingereza kushiriki michuano ya Uero.
Games 34
Games started 34
Mins played 3,008
Assists 1
Goals 24
Chances created 41
Goals/game 0.71
Win rate 56%
Jamie Vardy
Nyota huyu amesaidia Leicester City kushika usukani wa kuongoza ligi ya Uingereza kwa pointi 73. Vardy ameshafanikiwa kufunga magoli 22 akishika nafasi ya pili nyuma ya Harry Kane wa Tottenham.
Games 34
Games started 34
Mins played 2,959
Assists 6
Goals 22
Chances created 47
Goals/game 0.65
Win rate 62%
Wayne Rooney
Rooney ndiye nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza na tayari anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote kwenye timu ya taifa akifunga magoli 51. Japo kwa msimu huu anaonekana kutofanya vizuri sana kwenye timu yake ya Manchester United na majeraha yaliyomuandama ambayo yalimfanya kukaa nje ya uwanja kwa muda kidogo.
Games 23
Games started 22
Mins played 1,972
Assists 4
Goals 7
Chances created 34
Goals/game 0.30
Win rate 44%
Daniel Sturridge
Japo kipindi cha nyuma alionekana kutofanya vizuri kwenye timu ya Liverpool, Sturridge kwa sasa ameonekana kuwa ni mmoja wa washambuliaji muhimu kwenye timu hiyo. Kwa muda mrefu hakuwepo kwenye timu ya taifa ya Uingereza kwa sababu ya kupata majeraha yaliyomfanya aweze kukaa nje wa muda mrefu.
Games 10
Games started 8
Mins played 673
Assists 1
Goals 6
Chances created 4
Goals/game 0.60
Win rate 50%
Danny Welbeck
Welbeck ni mmoja kati ya washambuliaji wenye uwezo mkubwa wa kurudi nyuma na kukaba wakati timu inashambuliwa. Japo amekuwa hayupo fiti kwa muda mrefu kutokana na kuwa nje ya uwanja kwa majeraha ya muda mrefu, kwa sasa Welbeck ameonekana kurudi na kuanza kufanya vizuri ingawa ameonekana hapati nafasi sana kwenye timu ya Arsenal.
Games 8
Games started 6
Mins played 501
Assists 2
Goals 3
Chances created 5
Goals/game 0.38
Win rate 38%
Andy Carroll
Kwa sasa Carroll ameonekana kuanza kurudi kwenye makali yake kama kipindi yupo timu ya Newcastle United kabla ya kuhamia Liverpool na kiwango chake kupotea. Hatrick yake kwenye mechi ya West Ham United dhidi ya Arsenal inamfanya Hodgson ajiulize mara mbili na kufikiria kuchanga karata yake vizuri.
Games 22
Games started 8
Mins played 1,010
Assists 1
Goals 8
Chances created 8
Goals/game 0.36
Win rate 41%
Marcus Rashford
Rashford amekuwa ni mmoja kati ya washambuliaji chipukizi wenye uwezo mkubwa wa kufunga magoli mazuri. Mpaka sasa Rashford ana umri wa miaka 18 ameonekana kuwa ni mmoja kati ya wachezaji tegemezi wa timu hiyo akiwa tayari kashafunga magoli 8 kwenye mashindano yote aliyoichezea timu ya Manchester United.
Games 7
Games started 7
Mins played 546
Assists1
Goals 4
Chances created 2
Goals/game 0.57
Win rate 71%