Michezo

Henry Joseph: Hali yawa tete Ulaya

 

Henry Joseph Shindika na klabu yake ya KongsvingerĀ  ya Norway hawana raha na maisha katika kipindi hiki kwani wapo kwenye hatari mbaya sana ya kushuka daraja. Kongsvinger imeonekana kutaka kuigaManyema Rangers ya Dar es salaam ambayo hupanda msimu huo huo na kushuka msimu huo huo kwenye ligi.

Timu hiyo inashika nafasi ya 15 kwenye ligi inayoshirikisha timu 16 wakati ikielekea ukigoni hivyo ni miujiza tu inasubiriwa ili kuona Kongsvinger yenye point 11 tu kubaki.

Mambo yalikuwa mabaya wiki iliyopita baada ya kuchapwa 5-2 ugenini na Valeranga hivyo kuzidi kujichimbia kaburi. Leo Henry anatarajiwa kuiongoza tena timu yake katika harakati za kujiepusha na balaa hilo la kushuka daraja wakati itakapo menyana na Tromsokuanzia.

Ikumbukwe Henry ndie mchezaji pekee wa Tanzania anaye cheza ligi kuu ulaya baada ya Haruna Moshi Boban kulikoroga Gefle If ya Sweden.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents