Michezo

Ferguson akaribia kumnasa Mbelgiji

Manchester United imeweka mezani kiasi cha paundi milion 13 ili kumnasa kiungo wa Ubelgiji Steven Defour, kocha wa United Alex Ferguson amekuwa shabiki wa mchezaji huyo wa klabu ya Standard kwa kipindi kirefu lakini alilazimika kusubiri hadi kupona maumivu ya mguu wake uliovunjika.

 

Defour ana mkatba hadi mwaka 2013 lakini wakala wake Paul Stefani amethibitisha kuwa Sir Alex amemtaka nyota huyo tangu alipompelekea barua mwezi Septemba wakati bado alikuwa akiangaika kupona mguu.

“Bado ana nia ya kumsajili,lakini tunalazimika kusubiri ofa yake kukubaliwa na Standard Liege.Pia kuna maombi mengine kutoka klabu za Hispania Italia na Ujerumani,lakini kila mmoja anataka kucheza katika ligi kuu ya England,” alisema Stefani.

Wakati huo huo kocha mpya wa Liverpool Hodgson anajiandaa kumuuza kiungo wa Argentina Javier Mascherano kwenda Inter Milan ili apate fedha za kutosha kufanya kazi ya kukisuka kikosi cha timu hiyo ya Anfield

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents