Michezo

Huddersfield Town yasalia ligi kuu Uingereza, yaondoa matumaini ya Chelsea kusalia ‘top four’

Klabu ya Huddersfield Town imefanikiwa kusalia ligi kuu nchini Uingereza baada ya hapo jana kutoka sare ya bao 1 – 1 dhidi ya Chelsea kwenye uwanja wa Stamford Bridge huku wakiwafanya vijana hao wa Conte kupoteza matumaini ya kuwemo ‘top four’ itakayowafanya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao.

Huddersfield walifanikiwa kuwa na ukuta imara zaidi hali iliyopelekea kufanikiwa kupata sare hiyo iliyowafanya kusalia ligi kuu nchini Uingereza kwa kuwa na jumla ya pointi 37 huku wakiwaacha Swansea City watakao hitaji mabao 10 kusalia na kumshusha Southampton, West Brom na Stoke City wakiburuza mkia kwenye msimamo wa  ligi hiyo.

Wafungaji kwenye mchezo huo wakiwa ni Laurent Depoitre akiipatia timu yake ya Huddersfield dakika ya 50 na Marcos Alonso akiisawazishia Chelsea dakika ya 60.

Kwa matokeo hayo yanamfanya meneja wa Chelsea, Antonio Conte kuiyombea timu ya Brighton kuifunga Liverpool kwenye dimba la Anfield kwenye mchezo wa mwisho na yeye kuibuka na ushindi mbele ya Newcastle siku ya Jumapili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents