Promotion

Jay Dee kumuimbia Nelson Mandela

Lady Jay Dee a.k.a Jide antarajia kutumbuiza katika sherehe yakuzaliwa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini mheshimiwa Nelson Mandela ambayo inatarajiwa kufanyika jijini London nchini Uingereza mwezi Juni tarehe 27 mwaka huu

Lady Jay Dee pamoja na mkurugenzi wa masoko wa Celtel Tanzania,Margaret Kasitany
Lady Jay Dee pamoja na mkurugenzi wa masoko wa Celtel Tanzania, Margaret Kasitany

 

 

 

Lady Jay Dee a.k.a Jide antarajia kutumbuiza katika sherehe yakuzaliwa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini mheshimiwa Nelson Mandela ambayo inatarajiwa kufanyika jijini London nchini Uingereza mwezi Juni tarehe 27 mwaka huu.

 
Akizungumzia Hilo Mkurugenzi wa masoko wa Celtel, Margast Konsitany alisema alipokuwa akizindua promosheni mpya ya utuma ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu ya mkononi kumtakia kheri Nelson Mandela katika shereha hiyo ya kutimiza miaka 90 tangu alipozaliwa.

 
Tamasha hilo linalotarajiwa kuhudhuriwa na watu 46, 664 na kutizamwa na watu bilioni 1 duniani kote kupitia vituo mbali mbali vya luninga.

 

 

 

“Celtel Tanzania imeanzisha promosheni hii kutokana na kampuni mama ya Zain Group kudhamini tamasha hilo la kimataifa la kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Nelson Mandela. Zain Group inayoongoza kwa kwa kutoa huduma bora za mawasiliano ya simu barani Afrika na Mashariki ya Kati ni kampuni tanzu ya Celtel na itashiriki katika tukio hilo kubwa,” -Kositany.

 

 

 

Aliongeza kusema kuwa promosheni hiyo ya wiki tatu, itawawezesha wateja sita wa Celtel nao kuwa miongoni mwa watu watakaoshuhudia birthday ya Mandela.

 

 

 

Alitoa maelekezo kwa wateja hao ya kwamba wanachotakiwa kufanya ni kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuandika neno Mandela na kutuma kwenda namba 46664 na atajiwekea nafasi ya kushinda kwenda kwenye tamasha hilo au zawadi nyingine mbalimbali kutoka Celtel.

 

 

 

“Ujumbe huo utatumwa kwenda kwenye namba 46664 ndiyo aliyokuwa akitumia Mandela gerezani alipokuwa mfungwa kwenye gereza la Robben Island. Alikuwa mfungwa namba 466, kuanzia mwaka 1994,” alisema.

 

 

 

Kuhusiana na Jaydee, Mkurugenzi huyo alisema akiwa London, ataungana na wanamuziki wengine mahiri na kuwataja baadhi kuwa ni Papa Wemba wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Susana Owiyo wa Kenya na wengine wengi zaidi na maarufu duniani kote.

 

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents