Tragedy

Jinsi mastaa wa Tanzania walivyokipokea kifo cha Sajuki

Sajuki 2
Baada ya kuugua kwa muda mrefu, hatimaye aliyekuwa muigizaji wa filamu nchini, Juma Kilowoko maarufu kama Sajuki amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu.

Sajuki alikuwa akitakiwa kurejea tena nchini India kwaajili ya kuendelea na matibabu ya tatizo lililokuwa likimsumbua ambapo jumla ya shilingi milioni 28 zilikuwa zikihitajika.

Hivi karibuni ilidaiwa kuwa alikuwa ameshakusanya shilingi milioni saba tu zilizotokana na michango ya watu na show alizokuwa akizifanya kukusanya fedha hizo. Show ya mwisho aliifanya jijini Arusha ambako alianguka kwenye stage.

Kifo hicho cha Sajuki kimepokelewa kwa masikitiko makubwa kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo mastaa wa Tanzania waliotumia mitandao ya kijamii kuelezea masikitiko yao.

Mwasiti Almas

Tunapolala na kuamka tunasema AHSANTE kwa mungu,tunapopoteza pia tunaowapenda tuseme AHSANTE… alichokileta ALLAH chini ya jua atakichukua

Salama A. Jabir

Mwenyezi Mungu Akusamehe Makosa Yako Ndugu Yetu Juma Kilowoko..Ucheshi Wako Ntaukumbuka Milele. Pumzika Kwa Amani Rafiki. #RIPSajuki

Jokate Mwegelo

Nimesikia hii habari sasa. Sad lakini kazi ya Mungu haina makosa tunazidi kumtumainia yeye na kumshukuru. Upumzike kwa amani sajuki. Amen!!

Zitto Zuberi Kabwe

Hali ya Afya ya Sajuki ndiyo ilinisukuma sana kuanza kusaidia wasanii nchini kupata kipato stahili na kazi Yao. Kifo chake kimeniondolea Mtu niliyemtazama kama kishawishi Cha Mimi kupigania haki za Watanzania walio kwenye entertainment industry. Sajuki left an indelible mark in my politics. Pumzika Kwa Amani Juma.

Masanja ā€Mkandamizaji

Duniani si nyumbani kwetu. Ni njia tu.

Hemedy Suleiman

R.I.P SAJUKI……..daaaaaah this is painful!!

Arnold Kayanda

Pamoja na kuwa Msiba wowote unanisikitisha ila wa Sajuki unanisikitisha zaidi kila napoikumbuka Historia yake na Mkewe!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents