Burudani

Jose Chameleone wa Uganda kui ‘badilisha’ bongo weekend hii

Msanii mkubwa wa Africa Joseph Mayanja a.k.a Dr Jose Chameleone kutoka Uganda anategemewa kutua Bongo weekend hii na kubadilisha hali ya hewa ya burudani kwa wakazi wa jiji la maraha Dar es salaam.

Jose-Chameleone

Chameleone ambaye pia ametajwa kuwania tuzo za ‘Africa Entertainment Awards’ 2013 zitakazofanyika mwisho wa mwezi huu nchini Canada, anategemewa kutumbuiza katika kiota kipya cha burudani Escape One kilichopo jijini Dar es salaam jumamosi hii (August 10).

Chameleone ambaye alikuwa katika tour ndefu ya Marekani hivi karibuni, alifanikiwa pia kupata mtoto mwingine wa kiume (Amma Christian Mayanja) mwezi July mwaka huu na kufikisha idadi ya watoto wanne na mke wake Daniella.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents