Burudani ya Michezo Live

Kagame atangaza kung’atuka

Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Rwanda unaotarajiwa kufanyika Agosti 3 mwaka huu, Rais wa Rwanda Paul Kagame ameeleza kinaga ubaga kuwa ukomo wake wa kutawala ni mwaka 2024.

Tokeo la picha la kagame paul
Rais wa Rwanda, Paul Kagame

Rais Kagame amethibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wa Jeune Afrique kuwa awamu hii ya miaka saba ndiyo ya mwisho na Wanyarwanda wanatakiwa waanze kufikiria mtu mwingine atakayewaongoza baada ya mwaka 2024.

Inawezekana natakiwa niliangazie suala hili katika siku chache zijazo nitakapoanza mbio za urais. Kuna aina ya makubaliano kati yangu mimi na RPF-Inkotanyi kwa upade mmoja, na raia wa Rwanda kwa upande mwingine“,alisema Kagame na kuendelea kuweka wazi kuwa

Raia, kupitia kura ya maoni ya Disemba 2015, waliniomba niendelee kuwaongoza nikakubali, ila muda mwafaka wa kupumzika umewadia na waomba waanze kufikiri nje ya mimi baada ya miaka saba“,alisema Kagame kwenye mahojiano yake na mtandao wa Jean Afrique.

Kwa sasa hakuna shaka yoyote kuwa Rais Kagame atashinda uchaguzi wa urais mwaka huu na ni ushindi ambao umekuwa ukitabiriwa kwa muda mrefu na Wanyarwanda.

Mwaka 2015 Wanyarwanda wapatao milioni 4 ambao ni zaidi ya asilimia 70% ya wapiga kura, walipaza sauti zao kulitaka Bunge lirekebishe katiba ili Kagame apate nafasi ya kuendelea kutawala.

Bunge lilifanya hivyo ili limruhusu rais huyo ambaye ana umri wa miaka 59 kuwania awamu zingine mbili hadi mwaka 2034.

By Godfrey Mgallah

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW