Habari

Kampuni ya Apple kuwapa wateja wake offer ya charger original kwa nusu bei ili kushindana na feki za ‘mchina’

Kampuni ya Apple imetangaza programu ya kuuza USB power adaptors dunia nzima kwa punguzo la nusu ya bei ya kawaida ili kukabiliana na charger feki zinazofahamika zaidi kama ‘mchina’ hapa Tanzania.

Apple charger

Uamuzi huo wa Apple unafuatia ripoti iliyoonesha kuwepo kwa charger nyingi feki zisizokidhi ubora na usalama wa mteja, kwa mujibu wa taarifa ya Daily Mail.

Mfano mmoja wapo wa athari zitokanazo na charger feki ni lile la msichana wa China Ma Ailun (23) aliyefariki mwezi uliopita kwa kupigwa shoti wakati anaongea na simu ya iPhone iliyokuwa inachajiwa. Iligundulika kuwa charger aliyokuwa akitumia msichana huyo ilikuwa ni feki.

iphone5

Kampuni hiyo imesema katika kipindi cha ofa charger hizo ‘USB power adaptors’ zitapatikana kwa $10 ( 16,000 Tsh) kutoka bei ya kawaida inayofikia $23 (37,000 Tsh).

Charger hizo original za bei ya ofa zitaanza kupatikana kuanzia August 16 hadi October 18, na mteja yeyote atakayehitaji kununua atahitajika kuonesha serial number ya iPhone, iPad au iPod na kukabidhi charger yake (feki) ili apatiwe mpya.

Ipad

Kama wewe ni mmoja kati ya walioshtushwa na lile tukio la msichana aliyefariki akiwa anaongea na simu ya iPhone wakati anai charge, habari hii itakuwa inakuhusu hivyo chukua hatua ‘ng’wana wane’ (kwa sauti ya Masanja).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents